• HABARI MPYA

  Monday, February 04, 2019

  VINICIUS AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO LA LIGA REAL YASHINDA 3-0

  Kinda mwenye kipaji cha hali ya juu, Vinicius Junior mwenye umri wa miaka 18 akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la pili dakika ya 80 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Alaves, likiwa bao lake la kwanza kabisa katika La Liga katika uliofanyika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Mabao mengine yamefungwa na Karim Benzema dakika ya 30 na Mariano Diaz dakika ya 90 na ushei na kwa ushindi huo Real Madrid inafikisha pointi 42 katika mechi 22, ikiendelea kushika nafasi ya tatu nyuma ya Barcelona yenye pointi 50 na Atletico Madrid pointi 44 baada ya wote kucheza mechi 22 pia 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VINICIUS AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO LA LIGA REAL YASHINDA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top