• HABARI MPYA

  Saturday, February 09, 2019

  POGBA APIGA MBILI MAN UNITED YASHINDA 3-0 NA KUREJEA 'TOP FOUR'

  Kiungo Mfaransa, Paul Pogba akishangilia kwa kucheza dansi kake maarufu baada ya kuifungia Manchester United bao la kwanza dakika ya 14 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Fulham leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Craven Cottage mjini London. Pogba pia alifunga bao la tatu kwa penalti dakika ya 65 baada ya Le Marchand kumchezea rafu Juan Mata na bao la pili la Mashetani hao Wekundu limefungwa na Anthony Martial dakika ya 23 na kwa ushindi huo Man United inatimiza pointi 51 katika mechi ya 26 na kupanda hadi nafasi ya nne, ikiizidi kwa pointi moja tu Chelsea inayoangukia nafasi ya tano ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi 
     
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POGBA APIGA MBILI MAN UNITED YASHINDA 3-0 NA KUREJEA 'TOP FOUR' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top