• HABARI MPYA

  Saturday, February 09, 2019

  LIVERPOOL YAIPIGA BOURNEMOUTH 3-0 NA KUREJEA KILELENI

  Mshambuliaji Mmisri, Mohamed Salah akiondoka kwenda kushangilia baada ya kuifungia Liverpool bao la tatu dakika ya 48 akimalizia pasi ya Mbrazil Roberto Firmino katika ushindi wa 3-0 dhidi ya AFC Bournemouth kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield. Mabao mengine yamefungwa na Sadio Mane dakika ya 24 na Georginio Wijnaldum dakika ya 34 na kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 65 baada ya kucheza mechi 26, ikirejea kileleni sasa ikiizidi pointi tatu Manchester City ambayo kesho itamenyana na Chelsea Uwanja wa Etihad 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAIPIGA BOURNEMOUTH 3-0 NA KUREJEA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top