• HABARI MPYA

  Sunday, February 10, 2019

  BALE AFUNGA LA 100 REAL IKIICHAPA ATLETICO 3-1 WANDA METROPOLITANO

  Mshambuliaji Gareth Bale akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la tatu dakika ya 74 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji Atletico Madrid Uwanja wa Wanda Metropolitano mjini Madrid kufuatia kutokea benchi dakika ya 57 kuchukua nafasi ya  Vinicius Junior, hilo likiwa bao lake la 100 tangu ajiunge na klabu hiyo. Mabao mengine ya Real Madrid yamefungwa na Casemiro dakika ya 16 na Sergio Ramos dakika ya 42 kwa penalti wakati la Atletico Madrid limefungwa na Antoine Griezmann dakika ya 25 katika mchezo ambao wenyeji walimaliza pungufu baada ya kiungo wao, Thomas Partey kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano. Kwa ushindi huo, Real Madrid inafikisha pointi 45 katika mechi ya 23 na kupanda hadi nafasi ya pili, ikiizidi kwa pointi moja Atletico Madrid na ikizidiwa kwa pointi tano na vinara, Barcelona ambao pia wamecheza mechi 22 na watamenyana na Athletic Club 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALE AFUNGA LA 100 REAL IKIICHAPA ATLETICO 3-1 WANDA METROPOLITANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top