• HABARI MPYA

  Wednesday, February 06, 2019

  AZAM FC WASAWAZISHIWA BAO NA ALLIANCE FC DAKIKA YA MWISHO CHAMAZI, SARE 1-1

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Alliance FC ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Matokeo hayo yanamaanisha Azam FC imeshindwa kutumia mwanya wa Yanga kutoa sare ya 0-0 na Singida United jioni ya leo kupunguza idadi ya pointi inazozidiwa na vinara hao katika msimamo wa Ligi Kuu.
  Yanga SC yenye pointi 55, inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi saba zaidi ya Azam FC, ambayo hata hivyo ina mchezo mmoja mkononi.

  Katika mchezo wa usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Azam FC ilitangulia kwa bao la Joseph Mahundi dakika ya 79, kabla ya Dickson Ambundo kuisawazishia Alliance dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo huo.    
  Alliance FC yenye inafikisha pointi 32 katika mechi 25, ikiendelea kushika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu inayoshirikisha timu 20.
  Mechi nyingin za leo, Singida United imelazimishwa sare ya 0-0 na Yanga SC Uwanja wa Namfua, Tanzania Prisons imeshinda 2-1 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Kagera Sugar imefungwa 1-0 na Mbeya City Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Nayo Stand United imeifunga 2-0 Ndanda FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Lipuli FC imeshinda 1-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Samora, Iringa na JKT Tanzania imeshinda 3-1 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa michezo miwili, Simba SC wakiwa wenyeji wa Mwadui FC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na Mtibwa Sugar wakimenyana na African Lyon. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC WASAWAZISHIWA BAO NA ALLIANCE FC DAKIKA YA MWISHO CHAMAZI, SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top