• HABARI MPYA

  Sunday, February 10, 2019

  AGUERO APIGA HAT TRICK MAN CITY YAIFUMUA CHELSEA 6-0 ETIHAD

  Sergio Aguero akifurahi na kocha wake, Pep Guardiola wakati anatoka dakika ya 65 kumpisha mshambuliaji mwenzake, Mbrazil Gabriel Jesus baada ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad. Aguero alifunga mabao yake dakika za 13, 19 na la penalti dakika ya 56, wakati mabao mengine ya Mamn City yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya nne na 80 na Ilkay Gundogan dakika ya 25.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 65 katika mechi ya 27 ikipanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England kwa kuizidi wastani wa mabao tu Liverpool, ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi, wakati Chelsea inaangukia nafasi ya sita licha ya kuwa na pointi 50 sawa na Arsenal inayopanda nafasi ya tano kwa herufi baada ya kulingana pia na wastani wa mabao 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AGUERO APIGA HAT TRICK MAN CITY YAIFUMUA CHELSEA 6-0 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top