• HABARI MPYA

    Thursday, February 07, 2019

    AFRICAN LYON KUMENYANA NA SIMBA DAR BAADA YA HASARA MECHI YA KWANZA NA YANGA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya African Lyon imeamua kuurejesha Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Simba SC, zote za Jijini kutoka Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
    Kupitia kwa Rais wake, Rahim Kangenzi ‘Zamunda’, Lyon imeomba mchezo huo uliopangwa kufanyika Februari 19 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha urejeshwe Dar es Salaam.  
    Na Zamunda amesema sababu ya kubadili Uwanja wa nyumbani kwa mechi hiyo na nyingine, dhidi ya Azam FC ni ongezeko kubwa la gharama wachezapo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. 

    “Ikumbukwe ya kuwa African Lyon iliomba kutumia uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid kwa michezo mitatu ambayo ni dhidi ya Yanga Sports Club, Simba sports Club na Azam Football Club, lakini kutokana na ongezeko kubwa la gharama kila tuendapo Arusha, tumeona turudishe michezo iliyobaki katika Uwanja wa uhuru kwa manufaa ya kiuchumi ya klabu yetu,”amesema Zamunda.
    Zamunda amesema kwamba amefanya hivyo kwa sababu tayari kuna timu za Ligi Kuu zimebadili viwanja msimu huu baada ya kukwazwa kwa namna moja au nyingine na viwanja walivyovichagua awali.
    Ametolea mfano Azam FC ilitoa mechi zake ilizoomba zifanyike Uwanja wa Azam Ciomplex, Chamazi mjini Far es Salaam na kuzihamia Uwanja wa Taifa na JKT Tanzania iliomba kutumia Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kotoka Taifa.
    Nazo Ruvu Shooting iliomba kutumia Uwanja wa Taifa badala ya Mlandizi mkoa=ni Pwani kwa mechi dhidi ya Simba na Yanga, Mtibwa Sugar ikahamia Uwanja wa Jamhuri Morogoro mjini kutoka Manungu kwa mechi dhidi ya vigogo hao na Ndada FC iliwahi kihamishia mechi zake Uwanja wa Tafa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AFRICAN LYON KUMENYANA NA SIMBA DAR BAADA YA HASARA MECHI YA KWANZA NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top