• HABARI MPYA

  Thursday, January 10, 2019

  YANGA YAPEWA BIASHARA UNITED, AZAM FC NA PAMBA 32 BORA KOMBE LA TFF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Yanga SC itamenyana na Biashara United katika hatua ya 32 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Januari 25 na 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
  Katika droo iliyopangwa leo makao makuu ya Azam TV, mshindi kati ya Yanga SC na Biashara United atamenyana na mshindi kati ya Mighty Elephant na Namungo FC katika hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. 
  Nao mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar watamenyana na Maji Maji FC ya Songea, wakati vigogo wengine, Azam FC watamenyana na Pamba SC ya Mwanza.
  Kama ilivyo kwa Yanga, Azam FC nao watacheza nyumbani Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam na Mtibwa Sugar watacheza nyumbani Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Biashara United watarudi Dar es Salaam kumenyana tena na Yanga katika hatua ya 32 Bora kombe la TFF

  Mechi nyingine za hatua ya 32 Bora ni kati ya Mashujaa FC ya Kigoma iliyowatoa Simba SC dhidi ya Mbeya City FC, Friends Rangers na African Lyon, Mighty Elephant na Namungo FC, Alliance FC na La Familia, Dodoma FC na Transit Camp na Cosmo Politan dhidi ya Dar City.
  Mechi nyingine ni Reha FC na Boma FC, Rhino Rangers na Stand United, KMC na Pan Africans, Kagera Sugar Mbeya Kwanza, Polisi Tanzania na Lipuli FC, Kitayose na Coastal Union na Singida United dhidi ya JKT Tanzania. 
  Mechi zote za Raundi ya Nne, yaano 32 Bora zitafanyika kati ya Januari 25 na 28, 16 Bora kuanzia Februari 22 na 25 na Robo Fainali zitafanyika kati ya Machi 27 na 30 wakati fainali ya michuano hiyo mwaka huu itafanyika Uwanja wa Lulu mjini Lindi  
  Mshindi kati ya Mtibwa Sugar na Maji Maji FC atamenyana na mshindi kati ya KMC na Pan Africans na mshindi kati ya Azam FC na Pamba SC atamenyana na mshindi kati ya Rhino Rangers na Stand United.
  Mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar watamenyana na Maji Maji katika hatua ya 32 Bora michuano ya ASFC

  RATIBA HATUA YA 32 BORA ASFC
  Yanga SC V Biashara United
  Mtibwa Sugar V Maji Maji FC
  Azam FC V Pamba SC
  Mashujaa FC V Mbeya City FC
  Friends Rangers V African Lyon
  Mighty Elephant V Namungo FC
  Alliance FC V La Familia
  Dodoma FC V Transit Camp
  Cosmo Politan V Dar City
  Reha FC V Boma FC
  Rhino Rangers V Stand United
  KMC V Pan Africans
  Kagera Sugar V Mbeya Kwanza
  Polisi Tanzania V Lipuli FC
  Kitayose V Coastal Union
  Singida United V JKT Tanzania
  (Mechi zote zitafanyika kati ya Januari 25 na 28, 16)
  RATIBA HATUA YA 16 BORA ASFC
  Yanga SC/Biashara United V Mighty Elephant/Namungo FC
  KMC/Pan Africans V Mtibwa Sugar/Maji Maji FC 
  Azam FC/Pamba SC V Rhino Rangers/Stand United
  Friends Rangers/African Lyon V Mashujaa FC/Mbeya City FC
  Alliance FC/La Familia V Cosmo Politan/Dar City
  Polisi Tanzania/Lipuli FC V Dodoma FC/Transit Camp
  Reha FC/Boma FC V Kagera Sugar/Mbeya Kwanza
  Singida United/JKT Tanzania V Kitayose/Coastal Union
  (Mechi zitachezwa Februari 22 hadi 25)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAPEWA BIASHARA UNITED, AZAM FC NA PAMBA 32 BORA KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top