• HABARI MPYA

  Monday, January 07, 2019

  YANGA SC YAGONGWA 2-1 NA MALINDI NA KUTUPWA NJE KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  YANGA SC imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Malindi SC katika mchezo wa Kundi B usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Kwa matokeo hayo, Malindi SC inafikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu ikishinda mbili na kutoa sare moja, wakati Yanga inabaki na pointi zake tatu baada ya kucheza mechi tatu, ikishinda moja na kufungwa mbili.
  Malindi SC inaungana na Azam FC kujihakikishia kwenda Nusu Fainali ya michuano ya 13 ya Kombe la Mapinduzi na kwa ujumla zimeungana na Simba SC kutoka Kundi A, ambayo ilikuwa timu ya kwanza jana kuingia Nne Bora.    
  Katika mchezo wa leo, Yanga SC ndiyo waliokuwa wa kwanza kuoata bao dakika ya 35 kupitia kwa mshambuliaji wake Matheo Anthony Simon aliyefunga kwa kichwa akimalizia kona iliyopigwa na beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali.
  Malindi wakasawazisha bao hilo dakika ya 41 kupitia kwa Abdulsamad Kassim aliyefumua shuti kali kutoka umbali wa mita zaidi ya 30 ambalo lilimpita kipa wa Yanga, Ibrahim Hamid pamoja na kujaribu kuzuia.
  Kipindi cha pili pamoja na Yanga kukianza vizuri wakipambana kusaka bao la kusawazisha, lakini walijikuta wakipigwa wao bao la pili lililofungwa na Juma Hamad dakika ya 61.
  Kikosi cha Malindi SC kilikuwa: Ahmed Ali, Ali Juma, Muharami Issa, Samir Ali, Ibrahim Abdallah/ Adeyum Saleh dk54, Ali Kani, Mohammed Mosi, Abdulsamad Kassim, Khamis Makame/HaJji Wahaji dk82, Cholo Ali/Mohammed Mussa dk51 na Juma Hamad/Miskson Humbo dk65.
  Yanga; Ibrahim Hamid, Yassin Saleh, Mwinyi Hajji Mngwali, Cleophas Sospeter, Said Juma ‘Makapu’, Maka Edward, Shaaban Mohammed/Deus Kaseke dk80, Gustafa Simon/ Jaffar Mohammed dk69, Matheo Anthony, Faraji Kilaza/Cheda Hussein dk79 na Pius Buswita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAGONGWA 2-1 NA MALINDI NA KUTUPWA NJE KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top