• HABARI MPYA

  Sunday, January 13, 2019

  SIMBA QUEENS YAISHINDILIA YANGA PRINCESS 7-0 LIGI YA WANAWAKE KARUME LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Simba SC imeifunga Yanga Princess mabao 7-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya Simba Queens ifikishe pointi 13 baada ya kucheza mechi tano na kupanda kileleni mwa ligi hiyo, sasa ikiwazidi kwa pointi moja, mabingwa watetezi, JKT Queens ambao hata hivyo wana mchezo mmoja mkononi.
  Simba Queens sasa inalingana kwa pointi na mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo, Mlandizi Queens wakiwazidi kwa wastani wa mabao tu. 

  Mwanahamisi Omari ‘Gaucho’ (kulia) amefunga mabao manne leo Simba Queens ikiichapa Yanga Princess 7-0

  Katika mchezo wa leo, mabao ya Simba Queens yamefungwa na Amina Ramadhani, Mwanahamisi Omari ‘Gaucho’ manne, Frora Kayanda aliyejifunga na Amina Ally.
  Yanga Queens wanabaki na pointi zao sita baada ya kucheza mechi tano, wakiendelea kukamata nafasi ya saba kwenye ligi ya timu 12.
  Ushindi wa Simba Queens unakwenda sambamba na mafanikio ya kikosi cha wanaume cha klabu hiyo kwa sasa, jana tu ikitoka kushinda mechi yake ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika 3-0 dhidi ya JS saoura ya Algeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YAISHINDILIA YANGA PRINCESS 7-0 LIGI YA WANAWAKE KARUME LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top