• HABARI MPYA

  Friday, January 04, 2019

  SANE ALIPOIFUNGIA LA USHINDI MAN CITY IKIIPIGA 2-1 LIVERPOOL

  Leroy Sane akishangilia kishujaa baada ya kuifungia bao la ushindi Manchester City dakika ya 72 ikiilaza 2-1 Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Etihad. 
  Bao la kwanza la Machester City lilifungwa na Sergio Aguero dakika ya 40 kabla ya Roberto Firmino kuisawazishia Liverpool dakika ya 64.
  Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 50 na kuendelea kukamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sasa ikizidiwa pointi nne tu na vinara, Liverpool baada ya timu zote kucheza mechi 21 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SANE ALIPOIFUNGIA LA USHINDI MAN CITY IKIIPIGA 2-1 LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top