• HABARI MPYA

  Thursday, January 10, 2019

  RAMOS AFIKISHA MABAO 100 REAL MADRID IKISHINDA 3-0

  Sentahafu Sergio Ramos akishangilia baada ya kuifungia bao la kwanza Real Madrid pwa penalti dakika ya 44 jana usiku katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Leganes kwenye mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Mfalme Uwanja wa Santiago Bernabéu. Bao hilo linamfanya Ramos afikishe mabao 80 jumla Real Madrid na ukijumlisha na 17 aliyoifungia timu ya taifa ya Hispania na matatu klabu yake ya zamani, Sevilla anafikisha jumla ya mabao 100 ya kufunga hivyo kuwa beki wa kipekee katika ufungaji.
  Mabao mengine ya Real Madrid jana yalifungwa na Lucas Vázquez dakika ya 68 na Vinicius Junior dakika ya 77 na timu hizo zitarudiana Januari 16 Uwanja wa Manispaa ya Butarque mjini Leganés 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAMOS AFIKISHA MABAO 100 REAL MADRID IKISHINDA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top