• HABARI MPYA

  Tuesday, January 08, 2019

  PRISONS YAICHAPA MTIBWA 2-0 NA KUJIINUA KIDOGO KWENYE MSIMAMO WA LIGI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Tanzania Prisons imeanza harakat za kujiinua kutoka mkiani mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara  baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Ushindi huo wa kwanza chini ya kocha mpya Mohammed ‘Adolph’ Rishard aliyechukua nafasi ya Mohammed Abdallah ‘Bares’ aliyefukuzwa baada ya matokeo mabaya umetokana na mabao ya Salum Kimenya dakika ya 71 na Jumanne Elfadhil dakika ya 88.
  Na kwa ushindi huo wa pili tu wa msimu kwa timu hiyo ya Jeshi la Magereza, unaifanya Tanzania Prisons ifikishe pointi 15 baada ya kucheza mechi 20 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 19 kutoka ya mwisho, ya 20.

  Mtibwa Sugar baada ya kipigo cha leo inabaki nafasi ya sita na pointi zake 26 ikifikisha mechi 16 za kucheza, ikiwa nyuma ya Mbao FC yenye pointi 27 za mechi 10 na Lipuli FC pointi 29 za mechi 20.
  Ikumbukwe Yanga SC ndiyo inayoongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 50 za mechi 18, ikifuatiwa na Azam FC pointi 40 mechi 17 na mabingwa watetezi, Simba SC pointi 33 za mechi 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAICHAPA MTIBWA 2-0 NA KUJIINUA KIDOGO KWENYE MSIMAMO WA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top