• HABARI MPYA

  Friday, January 11, 2019

  NI SIMBA SC NA AZAM FC TENA FAINALI MAPINDUZI KWA MARA YA TATU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya Malindi SC usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Simba SC iliyotumia wachezaji wengi wa timu ya vijana leo, sasa itakutana na Azam FC katika Fainali ambayo mapema jioni ya leo iliichapa mabao 3-0 KMKM Uwanja wa Amaan, Zanzibar pia.
  Baada ya dakika 90 ngumu, mabeki Yussuf Mlipili, Mghana Asante Kwasi na kiungo Mohammed ‘Mo’ ibrahim wakaifungia SImba SC penalti zao huku beki mpya, Zana Coulibaly kutoka Burkina Faso akikosa kwa kupiga juu.
  Kwa upande wa Malindi, Abdulswamad Kassim pekee alifunga penalti yake, huku Ali Kani, Muharami Issa na Cholo Ali wakikosa wote.

  Tukio la kusisimua katika mchezo huo ni pale beki wa kati wa Simba, Paul Bukaba alipovunja kioo cha chumba cha waandishi wa habari baada ya shuti lake akiokoa hatari langoni mwake kwenda moja kwa moja katika dirisha la chumba hicho dakika ya 76.
  Katika mchezo uliotangulia jioni mabao ya Nahodha na beki Aggrey Morris dakika ya tisa, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 62 na mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 82 yakaipa Azam FC ushindi wa 3-0 dhidi ya KMKM.
  Sasa Azam na Simba zitakutana kwenye fainali ya michuano hiyo kwa mara ya tatu baada ya mwaka 2012 na 2017 walipofungwa na timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa.
  Kikosi cha Malindi SC kilikuwa: Ahmed Selemani, Ali Juma, Muharami Issa, Juma Ramadhan, Ibrahim Abdallah, Abdulswamad Kassim, Nassor Juma/Adeyun Saleh dk56, Ali Kani, Haji Wahaji, Juma Said/Mohammed Mussa dk54 na Juma Buluma.
  Simba: Ally Salim, Zana Coulibally, Asante Kwasi, Yusuph Mlipili, Paul Bukaba, Salum Shaaban, Dickson Mhilu, Mohammed Ibrahim, Adam Salamba, Abdul Suleiman na Yahya Mbegu/Andrew Michael dk70.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI SIMBA SC NA AZAM FC TENA FAINALI MAPINDUZI KWA MARA YA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top