• HABARI MPYA

  Wednesday, January 09, 2019

  NI AZAM FC NA KMKM, SIMBA SC NA MALINDI NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  AZAM FC itamenyana na KMKM katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi keshokutwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar wakati Simba SC itamenyana na Malindi SC.
  Hiyo ni baada ya Azam FC kushinda 2-1 dhidi ya Malindi SC usiku wa leo Uwanja wa Amaan katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Kombe la Mapinduzi.
  Kwa matokeo hayo Azam FC inamaliza kileleni mwa Kundi B ikifuatiwa na Malindi, wakati SImba SC imeongoza Kundi A ikifuatiwa na KMKM.

  Katika mchezo wa leo usiku, mabao ya Azam FC yamefungwa na beki na Nahodha Aggrey Morris dakika ya 26 na mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma dakika ya 76, wakati la Malindi limefungwa na Abdulsamad Kassim dakika ya 87.
  Nusu Fainali ya kwanza itaikutanisha Azam na KMKM Saa 10:15 jioni na ya pili ni kati ya Simba SC na Malindi Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI AZAM FC NA KMKM, SIMBA SC NA MALINDI NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top