• HABARI MPYA

  Thursday, January 10, 2019

  NAIBU SPIKA WA BUNGE DK TULIA MGENI RASMI SIMBA NA JS SAOURA JUMAMOSI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson ndiye atakuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na JS Saoura ya Algeria Jumamosi.
  Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Sunday Manara kwa Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam imesema kwamba Naibu Spika, Dk Tulia ataongoza maelfu ya Watanzania na mashabiki wa Simba kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Simba SC watakuwa wenyeji wa JS Saoura ya Algeria Jumamosi kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika na wapinzani wao hao wanatarajiwa kuwasili usiku wa leo.
  Simba SC itamkosa beki wake, Erasto Nyoni ambaye ni majeruhi aliyeumia Jumapili kwenye mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Viingilio katika mchezo wa Jumamosi ni Sh. 100,000 kwa watakaonunua tiketi za Platinum ambao watapatiwa huduma kukaa sehemu ya VIP A, Wataacha gari zao hoteli ya Serena na kuchukuliwa na basi maalum kwenda na kurudi Uwanja wa Taifa wakisindikizwa na Polisi, watapewa jezi mpya za Simba na Watapata viburudisho na vinywaji wakiwa uwanjani, Sh. 10,000 kwa VIP B na Sh. 5,000 kwa mzunguko.
  Mbali na Simba SC na JS Saoura, timu mpya ya mshambuliaji Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu timu nyingine katika kundi hilo ni Al Ahly ya Misri na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambazo zitamenyana pia Jumamosi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAIBU SPIKA WA BUNGE DK TULIA MGENI RASMI SIMBA NA JS SAOURA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top