• HABARI MPYA

  Saturday, January 05, 2019

  LIPULI YAIPIGA 2-1 COASTAL UNION IRINGA NA KUPANDA NAFASI YA NNE LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  TIMU ya Lipuli FC imeutumia vyema Uwanja wa nyumbani wa Samora mjini Iringa baada ya kuichapa mabao 2-1 Coastal Union ya Tanga jioni ya leo. 
  Pongezi kwa mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Miraji Athuman ‘Madenge’ aliyeifungia Lipuli FC bao la ushndi dakika ya 68.
  Na hiyo ni baada ya mshambuliaji, Ayoub Lyanga kuifungia bao la kusawazisha Coastal Union dakika ya 58, kufuatia nyota wa zamani wa Azam FC, Seif Abdallah Karihe kuanza kuwafungia wenyeji, Lipuli FC dakika ya 45 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Lipuli FC inayofundishwa na kocha Suleiman Abdallah Matola, mchezaji wa zamani wa Simba inafikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 20 na kupanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu kutoka ya tano.

  Lipuli sasa ipo nyuma ya vigogo, Simba SC ambao ndiyo mabingwa watetezi wenye pointi 33 za mechi 14, Azam FC pointi 40 za mechi 17 na Yanga SC pointi 50 za mechi 18.
  Coastal Union inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Juma Mgunda baada ya kipigo cha leo inabaki nafasi ya tisa na pointi zake 25 za mech 18.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Mbao FC imelazimishwa sare ya 0-0 na mahasimu wao wa Jiji, Alliance FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIPULI YAIPIGA 2-1 COASTAL UNION IRINGA NA KUPANDA NAFASI YA NNE LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top