• HABARI MPYA

  Friday, January 04, 2019

  LIGI YA SOKA YA UFUKWENI KUCHEZWA FEBRUARI HADI APRILI COCO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KATIKA jitihada za kukuza kiwango cha soka ya ufukweni, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeamua kuanzisha Ligi Kuu ya soka la ufukweni Tanzania Bara (BSL) inayotarajiwa kuanza Februari 9 hadi Aprili 14, mwaka huu, 2019.
  Ligi hiyo itakua inachezwa kwenye Uwanja wa COCO BEACH uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam kila Jumamosi na Jumapili kuanzia saa 8 mchana mpaka 12 jioni. 
  Taarifa ya Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo leo imesema kwamba kuelekea kwenye Ligi hiyo shirikisho hilo limeanza kusajili klabu zenye sifa na vigezo kwa ajili ya kushiriki.
  Ndimbo amesema kwamba Fomu za usajili zinapatika katika ofisi za TFF Makao Makuu, Karume, Ilala Dar es Salaam kwa ada ya shilingi laki moja (100,000).
  Amesema kila timu itapatiwa mipira miwili ya soka la ufukweni kutoka TFF baada ya kukamilisha usajili na kulipa Ada ya usajili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIGI YA SOKA YA UFUKWENI KUCHEZWA FEBRUARI HADI APRILI COCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top