• HABARI MPYA

  Thursday, January 10, 2019

  KIPA MSTAAFU KONGO, KIDIABA MBUNGE MPYA UPPER KATANGA

  KIPA mstaafu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Robert Kidiaba Muteba, maarufu kwa ushangiliaji wake wa kiruka kichura chura enzi zake amechaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Upper Katanga nchini mwake.
  Kidiaba, ambaye enzi zake anacheza pamoja na umahiri wa kuokoa michomo pia alikuwa kipenzi cha mashabiki kwa staili yake ya kushangilia kwa kuruka kichura chura sasa ndiye Mbunge mpya wa Upper Katanga.
  Kidiaba kwa sasa ni Kocha Msaidizi wa klabu aliyoichezea kwa muda mrefu, TP Mazembe ya Lubumbashi, DRC.

  Enzi zake akiwa na TP Mazembe, aliisaidia klabu hiyo kigogo cha Kongo kushinda mataji matatu ya Ligi y Mabingwa Afrika kuanzia mwaka 2009 hadi 2015.
  Kidiaba mwenye umri wa miaka 42 sasa, alistaafu soka ya ushindani mwaka 2015 na kuhamia kwenye siasa akijiunga na chama cha upinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (NPDD).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA MSTAAFU KONGO, KIDIABA MBUNGE MPYA UPPER KATANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top