• HABARI MPYA

  Wednesday, January 09, 2019

  DROO YA HATUA YA 32 BORA KOMBE LA TFF KUFANYIKA KESHO AZAM TV

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  DROO ya Hatua ya 32 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajiwa kufanyika kesho mjini Dar es Salaam.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo amesema mjini Dar es Salaam kwamba droo hiyo ya Raundi ya Nne ya michuano hiyo itafanyika makao makuu ya Azam Tv, Tabata mjini Dar es Salaam kuanzia Saa 5:00 asubuhi.
  Timu zilizofanikiwa kufuzu katika hatua hiyo ni pamoja na mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar, Yanga SC, Azam FC, Lipuli FC, KMC, Coastal Union, Kagera Sugar, Mbeya City, Stand United, JKT Tanzania, Singida United, Alliance FC na African Lyon.

  Nyingine ni Biashara United, Boma, Namungo, Mbeya Kwanza, Friends Rangers, Majimaji FC, Dodoma FC, Pamba SC, Rhino Rangers, Reha FC, Dar City, Polisi Tanzania, Mashujaa, Transit Camp, The Mighty Elephant, Cosmopolitan, Kitayosce, La Familia FC na Pan African. 
  Kwa mwaka wa pili mfululizo, vigogo wa soka nchini Simba SC wametolewa mapema tu katika hatua ya timu 64 wakifungwa 3-2 na Mashujaa ya Kigoma, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DROO YA HATUA YA 32 BORA KOMBE LA TFF KUFANYIKA KESHO AZAM TV Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top