• HABARI MPYA

  Saturday, January 05, 2019

  CHIRWA APIGA MBILI AZAM FC YAICHAPA YANGA SC 3-0 KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  TIMU ya Azam FC imeendeleza ubabe kwa Yanga SC kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuitandika mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi B usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa aliifunga mabao mawili timu yake ya zamani dakika za 33 na 60, wakati bao linguine lilifungwa na kiungo Mghana, Ennock Atta-Agyei dakika ya 40.
  Azam FC inafikisha pointi nne baada ya ushindi huo kufuatia sare ya 1-1 na Jamhuri ya Pemba katika mchezo wa kwanza na kupanda kileleni mwa Kundi B.
  Yanga SC baada ya kipigo cha leo inaangukia nafasi ya tatu, nyuma ya Azam na Malindi zenye pointi nne kila moja, wakati timu nyngine katika kundi hilo, Jamhuri ya tatu kwa pointi yake moja sawa KVZ inayoshika mkia.     
  Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili, Jamhuri ikianza kumenyana na KVZ Saa 10:15 jioni Kundi B na baadaye KMKM wakimenyana na Simba SC Kundi A Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, kama kawaida 
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Razak Abalora, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Moris, Stephan Kingue, Joseph Mahundi/Ramadhani Singano dk78, Mudathir Yahya, Obrey Chirwa/Donald Ngoma dk79, Tafadzwa Kutinyu/Salmin Hoza dk66 na Enock Atta-Agyei/Iddi Kipagwile dk85.
  Yanga SC; Ibrahim Hamid, Yassin Saleh, Mwinyi Mngwali, Cleophas Sospeter, Said Juma ‘Makapu’, Maka Edward, Deus Kaseke, Gustafa Simon/Faraj Kilaza dk85, Matheo Anthony, Pius Buswita na Shaaban Mohammed. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHIRWA APIGA MBILI AZAM FC YAICHAPA YANGA SC 3-0 KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top