• HABARI MPYA

  Friday, January 11, 2019

  AZAM FC YAINGIA FAINALI MAPINDUZI KWA MARA YA TANO, YA TATU MFULULIZO

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  AZAM FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KMKM jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Ushindi huo umetokana na mabao ya Nahodha na beki Aggrey Morris dakika ya tisa, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 62 na mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 82.
  Sasa Azam FC itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili itakayochezwa usiku kati ya Malindi SC na Simba SC Uwanja wa Amaan pia, Zanzibar.
  Hii inakuwa mara ya tano na mara ya tatu mfululizo kwa Azam FC kufika fainali ya michuano hiyo tangu ianzishwe mwaka 2007, baada ya awali kufika fainali katika miaka ya 2012, 2013, 2017 na 2018.
  Na katika miaka yote ambayo Azam FC imefika fainali imeweza pia kutwaa taji hilo, 2012 na 2017 ikiifunga Simba SC, 2013 ikiifunga Tusker FC ya Kenya na 2018 ikiifunga URA FC ya Uganda.
  Kikosi cha KMKM kilikuwa; Nassor Abdallah, Hafidh Mohammed, Hassan Choum, Makame Haji, Richard Jovit, Brown Bruno/Salum Mussa dakika 90, Ibrahim Khamis, Isihaka Said/Salum Said dakika ya 56, Mussa Ali,Iliasa Suleiman/Salum Akida dakika 56 na Ventiraus John
  Azam FC; Razak Abalora, Nicolas Wadada, Bruce Kangwa/ Hassan Mwasipili dakika 75, Yakubu Mohammed, Agrey Morris/Lusajo Mwaikenda dakika 85, Stephan Kingue, Mahundi Joseph/ Donald Ngoma dakika 45, Mudathir Yahya, Obrey Chirwa, Salum Abubakar/Novatus Dissmas dakika 84 na Enock Atta-Agyei.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAINGIA FAINALI MAPINDUZI KWA MARA YA TANO, YA TATU MFULULIZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top