• HABARI MPYA

  Monday, January 07, 2019

  AZAM FC YAICHAPA KVZ 2-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KVZ jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Ushindi huo unaifanya Azam FC, mabingwa watetezi wafikishe pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, wakishinda mbili na kutoa sare moja.
  Sasa wanafuatiwa na Malindi na Jamhuri, ambazo kila moja ina pointi nne, wakati Yanga ni ya nne kwa pointi zake tatu na KVZ inashika mkia ikiwa haina pointi.
  KVZ waliuanza vizuri mchezo wa leo na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 28 kupitia kwa Amour Bakar Ali akimalizia kazi nzuri ya Raphael Obi.
  Lakini Azam FC wakafanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 75 kupitia kwa mshambuliaji wake, Mzimbabwe Donald Ngoma aliyemelizia pasi ya mchezaji mwenzake wa zamani tangu Platinums FC ya Zimbabwe na Yanga ya Dar es Salaam, Mzambai Obrey Chirwa.
  Chirwa akatanua akaunti yake ya mabao kwenye michuano hii kwa kuifungia bao la pili Azam FC dakika 90 kwa kichwa akimalizia kona ya Ramadhani Singano 'Messi' ambayo ilipitia kwa Ngoma kabla ya kumfikia.
  Kikosi cha KVZ kilikuwa: Yakubu Bakari, Saleh Rajab, Hamid Salum, Iddi Mgeni, Juma Abdallah, Mohammed Abdallah, Suleiman Abdi, Raphael Obi, Amour Bakar, Makarani Makarani na Mohammed Nassor/Omary Khamis dk59.
  Azam FC; Razak Abalora, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Agrey Moris, Stephan Kingue, Iddi Kipagwile/Daniel Lyanga dk45, Mudathir Yahya/Donald Ngoma dk69, Obrey Chirwa, Salum Abubakar na Enock Atta-Agyei.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA KVZ 2-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top