• HABARI MPYA

  Sunday, January 13, 2019

  AL AHLY YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YAILAZA VITA 2-0

  TIMU ya Al Ahly ya Misri imeanza vyema hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana usiku Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
  Ushindi huo uliotokana na mabao ya Nasser Maher dakika ya 65 na Ali Maaloul kwa penalti dakika ya 79, unaifanya Al Ahly ianzie nafasi ya pili kwenye Kundi D, ikizidiwa bao moja la kufunga na Simba SC ya Tanzania ambayo nayo jana ilishinda 3-0 nyumbani dhidi ya JS Saoura ya Algeria.
  AS Vita jana ililazimika kucheza pungufu tangu dakika ya 36 baada ya beki wake, Dharles Mondia Kalonji kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kucheza rafu, ya kwanza akionyeshwa dakika ya 21.
  Simba SC sasa itasafiri kuwafuata AS Vita mjini Kinshasa Januari 19, wakati JS Saoura watakuwa wenyeji wa Ahly Januari 18 nchini Algeria.
  Naye mshambuliaji mpya wa Ismailia ya Misri, Mtanzania Yahya Zayd hakuwepo hata benchi jana timu yake hiyo ikichapwa 2-0 na wenyeji, TP Mazembe katika mchezo wa Kundi C mjini Lubumbashi.
  Zayd amejiunga na Ismailia wiki iliyopita kutoka Azam FC na bila shaka taratibu za usajili zimemkwamisha kuanza kuitumikia klabu yake mpya. 

  Al Ahly wameanza vyema michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana kwa kuichapa AS Vita 2-0

  MATOKEO MECHI ZA KWANZA 16 BORA
  Januari 12, 2019
  Simba SC 3-0 JS Saoura Kundi D
  Al Ahly 2-0 AS Vita Kundi D
  Platinum 0-0 Orlando Pirates Kundi B
  TP Mazembe 2-0 Ismailia Kundi C
  Januari 11, 2019
  Lobi Stars 2-1 Mamelodi Sundowns Kundi A
  Horoya 1-1 Esperance Kundi B
  Wydad Casablanca 5-2 ASEC Mimosas Kundi A
  Club Africain 0-1 CS Constantine Kundi C
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YAILAZA VITA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top