• HABARI MPYA

  Thursday, December 06, 2018

  TFF YAUSOGEZA MBELE MKUTANO WAKE MKUU WA MWAKA HADI MWAKANI ILI IUNGANISHE NA UCHAGUZI MDOGO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyokutana Novemba 29,2018 imesogeza Mkutano Mkuu uliokuwa ufanyike Desemba 30,2018 Mkoani Arusha na sasa sasa utafanyika Februari 2, mwakani.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo amewaambia Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam kwamba sababu ya kusogezwa kwa Mkutano Mkuu ni kuendana na Kalenda ya Uchaguzi mdogo uliotangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho hilo.
  Amesema uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji anayewakilisha Lindi na Mtwara na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji anayewakilisha Simiyu na Shinyanga na zoezi la kuchukua na kurudisha fomu lililoanza juzi litafikia tamati Jumapili.
  Viongozi wakuu wa TFF, Rais Wallace Karia na Makamu wake, Michael Wambura (kulia) 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAUSOGEZA MBELE MKUTANO WAKE MKUU WA MWAKA HADI MWAKANI ILI IUNGANISHE NA UCHAGUZI MDOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top