• HABARI MPYA

  Wednesday, December 05, 2018

  TANZANIA YATUA MISRI TAYARI KUSHIRIKI FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA ZA SOKA LA UFUKWENI KUANZIA IJUMAA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni kimewasili nchini Misri tayari kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kufanyika katika mji wa Sharm El Sheikh kuanzia Desemba 8 hadi 14, mwaka huu.
  Tanzania inayofundishwa na kocha Boniface Pawasa imepangwa Kundi B pamoja na mabingwa watetezi, Senegal, Nigeria na Libya, wakati Kundi A lina timu za Misri, Morocco, Madagascar na Ivory Coast.
  Tanzania itafungua dimba na Libya Jumamosi, yaani Desemba 8, kabla ya kumenyana na Senegal Jumapili (Desemba 9) na kumaliza na Nigeria Jumatatu (Desemba 10).

  Wachezaji wa Tanzania wakipata chakula leo mjini Cairo, Misri baada ya kuwasili tayari kushiriki Fainali za Afrika za soka la ufukweni

   Nusu Fainali zitafuatia Desemba 12 na Fainali Desemba 14, wakati bingwa na mshindi wa pili watajikatia tiketi ya kwenda kushiriki Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Paraguay.
  Kikosi cha Tanzania kilichowasili Misri leo kinaundwa na; Ibrahim Hamad Abdallah, Juma Sultan Ibrahim, Rolland Narcise Msonjo, Samuel John Mauru, Yahya Said Tumbo, Jaruphu Rajab Juma, Ahmada A Ahmada, Alfa Wilfred Tindise, Kashiur Salum Said, Mohammed Makame Silima, Juma Kaseja Juma na Mbwana Mshindo Mussa.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YATUA MISRI TAYARI KUSHIRIKI FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA ZA SOKA LA UFUKWENI KUANZIA IJUMAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top