• HABARI MPYA

  Monday, December 10, 2018

  RIVER PLATE WAIPIGA BOCA JUNIORS NA KUBEBA COPA LIBERTADORES

  Wachezaji wa River Plate wakifurahia na taji lao la Copa Libertadores baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya wapinzani wao wa Argentina, Boca Juniors katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Amerika Kusini usiku wa jana Uwanja wa Bernabeu mjini Madrid, Hispania. Mabao ya River Plate yalifungwa na Lucas Pratto dakika ya 68, Juan Quintero dakika ya 109 na Gonzalo Martinez dakika ya 120 na ushei baada ya Boca Juniors kutangulia kwa bao la Dario Benedetto dakika ya 44.
  Kwa matokeo hayo, River Plate wanabeba Copa Libertadores kwa ushindi wa jumla wa 5-3, kufuatia sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Novemba 11 Uwanja wa Alberto Jose Armando Uwanja wa Ciudad de Buenos Aires 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RIVER PLATE WAIPIGA BOCA JUNIORS NA KUBEBA COPA LIBERTADORES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top