• HABARI MPYA

    Monday, December 10, 2018

    NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JOHN KANYASU AITAKA TANAPA KUTUMIA CHAMA CHA RIADHA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA

    Na Alphonce Kabilondo, GEITA
    NAIBU  Waziri wa Maliasili na Utalii John Costantine Kanyasu amelitaka shirika la hifadhi za Taifa nchini  TANAPA kukitumia chama cha riadha nchini kutangaza vivutio vinavyo patikana kwenye hifadhi za Taifa pamoja na wanariadha wakubwa wa ndani na nje ya nchi wakimbiza beiskeli maarufu .
    Naibu Waziri ametoa kauli hiyo Mjini Chato Mkoani Geita wakati akikabidhi zawadi mbali mbali vyeti pamoja na fedha kwa washindi wa riadha ,mbio za baiskeli  walioshiriki bonaza la  Rubondo Marathon lililokuwa limeandaliwa na  hifadhi ya kisiwa cha Rubondo kwa ufadhili wa shirika la hifadhi za Taifa nchini TANAPA  na shirika la Umeme Tanesco Wilayani Chato .
    Kanyasu alisema kuwa shirika hilo halina budi kukitumia chama cha riadha nchini pamoja na wanariadha wakubwa , wakimbiza baiskeli maarufu wanaotambulika na kuwataka walioshinda kwenye bonaza la Rubondo Marathon kuwenda kuwa  mabalozi wazuri wakukitangaza kisiwa cha hifadhi ya Rubondo pia amelitaka shirika hilo kuboresha bonaza hilo na kwamba lifanyike kila mwaka kwa kuzingatia sheria na kanuni za riadha na mbio za beiskeli kuepuka kupata washindi wasio stahili.



    Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii John Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi Shamim Ramadhani mshindi wa mbio za kilometa kumi baada ya kuibuka mshindi kwenye bonaza la Rubondo Marathon 


    Aidha Masunga Duba aliyeibuka mshindi wa kwanza kwa wanaume kwenye mbio za beiskeli kutoka Mkoa wa Simiyu na hivyo kuibuka na kitita cha shilingi milioni moja akatumia kutoa kili chao kwa serikali kuwa iwawezeshe kupata baiskeli za kisasa zitakazo wawezesha kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa na kuitanza Tanzania ambapo mshindi wa riadha kilometa kumi Shamim Ramadhani amesema kuwa mashindano hayo yaweendelevu ambapo amewashauri washiriki wenzake kutokata tama .
    Mratibu wa bonaza hilo  Alieth Ngaiza akitoa taarifa fupi kwa Naibu Waziri huyo amesema kuwa bonaza liliasisiwa na wasomi wa chuo kikuu wasio na ajira kikundi cha mahusiano ya jamii MAMAJA  lengo likiwa ni kuhamasisha kurinda maliasili na hifadhi za Taifa pamoja na utalii wa ndani na kwamba bonaza limehusisha washiriki kutoka mikoa ya Simiyu ,Mwanza, Shinyanga ,Arusha na wenyeji Mkoa wa Geita .
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JOHN KANYASU AITAKA TANAPA KUTUMIA CHAMA CHA RIADHA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top