• HABARI MPYA

  Tuesday, December 04, 2018

  MTIBWA SUGAR KUMENYANA NA KCCA KAMPALA DESEMBA 14 BAADA YA KUITUPA NJE NORTHEN DYNAMO LEO SHELISHELI

  Na Mwandishi Wetu, MAHE
  TIMU ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kwenda Raundi ya pili ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Northen Dynamo jioni ya leo Uwanja wa Linite, Glacis kisiwa cha Mahe nchini Shelisheli.
  Kwa ushindi huo uliotokana na bao pekee la kiungo Haroun Chanongo, Mtibwa Sugar inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-0, baada ya kushinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Eric Manirakiza aliyesaidiwa na washika vibendera, Hervé Kakunze na Ramadhani Nijimbere, wote wa Burundi, Northen Dynamo walijitahidi kuwabana wapinzani wao.

  Ikumbukwe katika mchezo wa kwanza shujaa wa Mtibwa Sugar alikuwa ni mshambuliaji Jaffar Salum Kibaya aliyefunga mabao matatu, huku bao la nne likifungwa mtokea benchi Riffat Khamis Msuya.
  Sasa Mtibwa Sugar itamenyana na KCCA ya Uganda inayoanzia Raundi ya Kwanza na mechi ya kwanza itafanyika Desemba 14 mjini Kampala kabla ya timu hizo kurudiana wiki moja baadaye Dar es Salaam.
  Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Kombe la Shirikisho, Zimamoto wametupwa nje licha ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kaizer Chiefs jioni ya leo Uwanja wa Amaan, kisiwa cha Unguja.
  Zimamoto inatupwa nje kwa jumla ya mabao 5-2 baada ya kufungwa 4-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Port Elizabeth.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR KUMENYANA NA KCCA KAMPALA DESEMBA 14 BAADA YA KUITUPA NJE NORTHEN DYNAMO LEO SHELISHELI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top