• HABARI MPYA

  Wednesday, December 05, 2018

  MHASIBU AIAMBIA MAHAKAMA MALINZI ALIIKOPESHA TFF DOLA ZA KIMAREKANI 41,000 NA SH. MILIONI 22

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHAHIDI wa tisa katika kesi utakatishaji fedha inayowakabili viongozi wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania, Sereck Mesack (68) amesema kwamba aliyekuwa Rais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi aliwahi kuikopesha taasisi hiyo dola za Kimarekani 41,000 mwaka 2016.
  Mesack, ambaye ni Mhasibu wa zamani wa TFF, amesema hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu mjini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo.
  Mesack alisema pamoja na dola 41,000 Malinzi pia aliikopesha TFF Sh. Milioni 22, fedha ambazo zilitumika kulipia posho na gharama za kuipeleke timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys nchi za Rwanda na Kongo.

  Mbele ya wakili Mwandamizi wa Serikali, Shadrack Kimaro aliyekuwa akisaidiana na Wakili wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Nikson Shayo, Mesack alisema Februari 9, 2016 kitabu cha kutolea risiti namba 00710-00750 kilionyesha Malinzi aliikopesha TFF Sh Milioni 10 na risiti ilisainiwa na Flora Rauya ambaye pia ni mshitakiwa katika kesi hiyo.
  Shahidi huyo aliyeanza kazi TFF mwaka 1985 na kustaafu Januari 2018, alida katika kitabu cha risiti namba 00801-00850 Mei 9, 2016 Malinzi aliikopesha TFF Dola za Marekani 8,000 na katika tarehe hiyo hiyo, mshitakiwa huyo wa kwanza alikopesha shirikisho hilo Dola za Marekani 7,000.
  ‘’Katika kitabu cha risiti namba 00851-00900, risiti namba 00870 ya Mei 27, 2016 kilionyesha kuwa Sh 5milioni  zilipokelewa kutoka kwa Malinzi ikiwa kama mkopo na Juni 16, mwaka huo huo, risiti namba 00931 ilionyesha kuwa Malinzi aliikopesha TFF Dola za Marekani 10,000,’’ alidai Mesack na kuongeza kuwa
  "Pia, Agosti 2, 2016, kitabu cha risiti namba 00947 kilionesha kuwa Dola za Marekani 1,000 zilipokelewa kutoka kwa Malinzi kwenda kwa Ayuob Nyenzi na P Rutayuga ambao walikwenda Afrika Kusini."Alida shahidi
  Mesack alida kitabu cha risiti namba 0010-01050, kilionyesha Septemba 21, 2016 Sh 3 milioni zilipokelewa kutoka kwa Malinzi kwenda kwa Timu ya Vijana chini ya miaka 17 ziliwa ni sehemu ya posho na alitoa Sh Milioni 7 kwenda ARS.
  Pia ilidai Septemba 22, 2016 Malinzi alitoa fedha ambazo ni Dola za Marekani 15,000 kwa ajili ya timu hiyo kama gharama za safari kwenda nchi za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC).
  ‘’Anayetoa fedha kwa mhasibu anapewa risiti na hiyo fedha inatakiwa kusomeka kwenye risiti ambazo zina nembo ya TFF, anuani na pia zinatakiwa zisomeke kwenye mfumo wa kompyuta na kwenye akaunti ambayo inahusiano na shirikisho hili,’’ alisema.
  Alisema kwamba, katika muamala mmoja kunatakiwa kuwa na nakala tatu ambapo ile nakala halisi anapewa muhusika na mbili zinabaki kwenye kitabu kama kumbukumbu kwenye kitabu cha risiti kinachopatikana kwenye ofisi ya mhasibu.
  Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 18, mwaka huu itakaendelea na ushahidi.
  Mbali na Malinzi, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa  Selestine(46),  Mhasibu wa TFF,  Nsiande  Mwanga(27), Meneja wa  Ofisi TFF, Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya.
  Kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 30 katika  kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa dola za Marekani 173,335 na Sh 43,100,000.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MHASIBU AIAMBIA MAHAKAMA MALINZI ALIIKOPESHA TFF DOLA ZA KIMAREKANI 41,000 NA SH. MILIONI 22 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top