• HABARI MPYA

    Sunday, December 02, 2018

    MBEYA CITY YAITANDIKA AFRICAN LYON 4-1 SOKOINE, KAGERA NAYOA YASHINDA, JKT YALAZIMISHWA SARE NA RUVU SHOOTING MBWENI

    Na Mwandishi Wetu, MBEYA
    TIMU ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya African Lyon ya Dar es Salaam jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
    Ushindi huo umetokana na mabao mawili mawili ya Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya pili nay a 20 na Eliud Ambokile dakika ya 23 na 28, wakati bao pekee la Lyon limefungwa na Adam Omary kwa penalti dakika ya 90.
    Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi 15 na kupanda hadi nafasi tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu kutoka ya saba, wakati Lyon inabaki na pointi zake 11 za mechi 14 katika nafasi ya 18 kwenye ligi ya timu 20.

    Mechi nyingine za Ligi Kuu leo,  bao pekee la Ramadhani Kapera dakika ya sita limeipa ushindi wa 1-0 Kagera Sugar dhidi ya Alliance FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
    Nayo JKT Tanzania imelamizimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ruvu Shooting katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Meja Isamhuyo huko Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
    Wageni, Ruvu Shooting walitangulia kwa la Alinanuswe Martin dakika ya 71 kabla ya wenyeji kusawazisha kupitia kwa Said Luyaya dakika ya 86.
    Ndanda FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mbao FC Uwanja wa Nangwanda SIjaona mjini Mtwara.
    Mchezo kati ya wenyeji, Lipuli FC na Biashara United ya Musoma mkoani Mara imeahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kuharibu mandhari ya Uwanja wa Samora mjini Iringa na sasa itachezwa kesho Saa 8:00 mchana.    
    Maana yake, kesho kutakuwa ne mechi mbili za Ligi Kuu, mwingine ukiwa ni kati ya Tanzania Prisons na Yanga SC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ambayo itaanza Saa 10:00 jioni. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YAITANDIKA AFRICAN LYON 4-1 SOKOINE, KAGERA NAYOA YASHINDA, JKT YALAZIMISHWA SARE NA RUVU SHOOTING MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top