• HABARI MPYA

  Wednesday, December 05, 2018

  KINDOKI ATUNGULIWA MABAO MAWILI YANGA SC YACHAPWA 2-1 MECHI YA KIRAFIKI SUMBAWANGA LEO

  Na Mwandishi Wetu, SUMBAWANGA
  KIPA Klaus Kindoki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo amefikisha mabao nane ya kufungwa Yanga SC katika mechi 10 tu alizocheza tangu asajiliwe Julai mwaka huu.
  Hiyo ni baada ya Yanga SC kuchapwa mabao 2-1 na wenyeji Sumbawanga United katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Mandela mjini humo.
  Mabao ya Sumbawanga United yalifungwa na Romano Nchimbi dakika ya sita na John Sabas ‘Boban’ dakika ya 61, wakati la Yanga SC lilifungwa na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko dakika ya 45.

  Klaus Kindoki leo amefikisha mabao nane ya kufungwa Yanga SC katika mechi 10 tu
  Kikosi cha Yanga SC kilichoanza leo dhidi ya Sumbawanga United Uwanja wa Mandela

  Mabao yote ya Sumbawanga United yalitokana na mashuti ya mbali na la Yanga Kamusoko alifunga kwa shuti la mpira wa adhabu. 
  Kikosi cha Yanga kimeondoka usiku wa leo mjini Sumbawanga kurejea Mbeya kuunganishe ndege ya ATC kesho jioni kurejea Dar es Salaam ambako Jumapili kitakuwa na mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Biashara United ya Mara.
  Katika mchezo huo, Yanga SC itawakosa wachezaji wake wawili nyota, viungo Mrisho Khalfan Ngassa anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu na Ibrahim Ajibu anayetumia adhabu ya kadi za njano.
  Kikosi cha Yanga SC leo Sumbawanga kilikuwa; Klasu Kindoki, Paulo Godfrey, Jaffar Mohammed, Cleophas Sospeter, Said Juma ‘Makapu’, Maka Edward, Pius Buswita, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Mrisho Ngassa, Matheo Anthony na Deus Kaseke.

  REKODI YA KLAUS KINDOKI YANGA
  1. Yanga SC 1-0 Mawenzi Market (Hakufungwa Kirafiki              Jamhuri Morogoro)
  2. Yanga SC 1-0 African Lyon (Hakufungwa Kirafiki Taifa)
  3. Yanga SC 4-3 Stand United (Alifungwa tatu na Felix                Kitenge Ligi Kuu Taifa)
  4. Yanga SC 1-0 Coastal Union (Hakufungwa Ligi Kuu                Taifa)
  5. Yanga SC 2-0 Mbao FC (Aliingiaa dakika ya 55 Beno              alipoukia, hakufungwa, Ligi Kuu Taifa)
  6. Yanga SC 1-0 African Lyon (Hakufungwa Kirafiki Uhuru)
  7. Yanga SC 1-1 Reha FC (Alifungwa moja kirafiki Uhuru)
  8. Yanga SC 1-1 Namungo FC (Alifungwa moja Kirafiki              Ruangwa)
  9. Yanga SC 2-1 Mwadui FC (Alifungwa moja akatolewa            kipindi cha pili, Ligi Kuu Shinyanga)
  10. Yanga SC 1-2 Sumbawanga United (Alifungwa mbili               kirafiki Sumbawanga)

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KINDOKI ATUNGULIWA MABAO MAWILI YANGA SC YACHAPWA 2-1 MECHI YA KIRAFIKI SUMBAWANGA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top