• HABARI MPYA

  Friday, December 07, 2018

  BORUSSIA DORTMUND UGENINI KWA SCHALKE 04 KWENYE RUHR DERBY

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KILA inapofika wikendi  basi wapenzi wa Soka wanajua tayari ni muda mwingine wa burudani yao wanayoipenda zaidi. Shauku ya kuwaona wachezaji wanaowapenda na kandanda la kuvutia, mahali sahihi ni ST World Football ambao watakuonyesha kandanda muda wote.
  Jumamosi hii katika Bundesliga, Schalke 04 watakuwa nyumbani dhidi ya Borrusia Dortmund ambao wanaongoza ligi huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote ndani ya Bundesliga tangu msimu huu ulipoanza. Borussia Dortmund wamefunga jumla ya mabao 37 huku Schalke wakifunga magoli 14 tu katika michezo 13 ya ligi na wanashikilia nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi ambayo Dortmund wanaongoza. Mchezo huo utarushwa MUBASHARA kupitia ST World Football HD saa11:30 jioni siku ya Jumamosi. Dortmund wanaonekana kukamilika sana katika safu ya kiungo na ushambuliaji ambayo inaongozwa na Marco Reus ambaye amaekuwa nje kwa muda akiuguza majeraha. Reus amefunga magoli 9 na kusaidia mengine 5 huku kinara wa magoli Paco Alcacer akiwa na magoli 10 ambayo 7 kati ya hayo amefunga akitokea benchi.
  Utakuwa mchezo mzuri sana ambapo Schalke 04 wanategemea kupata matokeo katika mtanange huo wa watani maarufu kama ‘River Derby’ dhidi ya kikosi imara cha Dortmund chini ya Kocha Lucian Fevre. Schalke 04 waliondokewa na kiungo wao tegemeo, Leon Goretzka ambaye alitimkia Bayern mwanzoni mwa Msimu huu, hawajafanya uwekezaji wakutosha kupambana na kasi ya vilabu vingine.
  Katika ligi ya Ufaransa wikendi hii, mchezo wa St Etienne dhidi ya Olympique Marseille utarushwa moja kwa moja kupititia ST World Football HD sambamba na taarifa ama usimulizi wa Kiswahili kutoka kwa wachambuzi makini kabisa.
  Wateja wa StarTimes wataweza kutizama mechi zote hizi kwa kulipia kifurushi cha Mwezi mzima cha MAMBO kwa TSH 14000 tu upande wa Antenna na SMART kwa Tsh 21000 kwa upande wa Dish. Katika msimu huu wa Siku kuu kila watakapolipia kifurushi cha MAMBO/SMART watabustiwa hadi kifurushi cha UHURU/SUPER upande wa Antenna na Dish.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BORUSSIA DORTMUND UGENINI KWA SCHALKE 04 KWENYE RUHR DERBY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top