• HABARI MPYA

  Tuesday, December 11, 2018

  DIRISHA DOGO LA USAJILI LIGI KUU TANZANIA BARA KUFUNGWA DESEMBA 15 WALIOTOLEWA KWA MKOPO NAFASI ZAO HAZIZIBWI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  DIRISHA Dogo la Usajili kwa Klabu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili Tanzania litafungwa Saa 5:59 usiku ya Desemba 15, mwaka huu.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo amesema kwamba klabu zote zinakumbushwa kutuma orodha ya wachezaji waliowaongeza katika dirisha dogo.
  Amesema wakati wa dirisha dogo klabu zinazoruhusiwa kuongeza idadi ya wachezaji ni zile ambazo hazikusajili wachezaji 30 wakati wa kipindi cha usajili wa dirisha kubwa.
  Mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa amesajiliwa Azam FC katika dirisha dogo 
  Ndimbo amesema kwamba klabu zilizotoa wachezaji kwa mkopo hazipati nafasi ya kusajili wachezaji wa kuziba nafasi hizo, bali zile zimewapa uhamisho wa moja kwa moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIRISHA DOGO LA USAJILI LIGI KUU TANZANIA BARA KUFUNGWA DESEMBA 15 WALIOTOLEWA KWA MKOPO NAFASI ZAO HAZIZIBWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top