• HABARI MPYA

  Monday, December 10, 2018

  AZAM FC YABANWA NA KMC UHURU, ZATOKA SARE 2-2 NA KUIACHIA NAFASI YANGA SC IJITANUE KILELENI LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam jioni ya leo.
  Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Azam FC na kufikisha 40 katika mechi ya 16, sasa wakizidiwa pointi moja tu na vinara, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi 15.
  KMC ilitangulia kwa bao la George Sangija dakika ya 18 kabla ya Azam FC kusawazisha kiungo Mzimbabwe, Tafadzwa Kutinyu dakika ya 45.

  KMC tena wakaitangulia Azam FC kwa bao la Rayman Mgungila dakika ya 63, kabla ya mshambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma kuisawazishia timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na family yake dakika ya 85.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Lipuli FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Mabao ya Lipuli ya kocha Suleiman Matola yalifungwa na Miraj Athumani ‘Madenge’ dakika za 36 na 43, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Said Dilunga dakika ya 90 na ushei.
  Kufuatia ushindi huo, Lipuli FC inafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 16 na kupanda kutoka nafasi ya 15 hadi ya 10 kwenye msimamo wa ligi, wakati Ruvu inayobaki na pointi zake 17 za mechi 16, inaporomoka kwa nafasi moja hadi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YABANWA NA KMC UHURU, ZATOKA SARE 2-2 NA KUIACHIA NAFASI YANGA SC IJITANUE KILELENI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top