• HABARI MPYA

  Tuesday, November 13, 2018

  TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 23 YAENDA KUCHEZA NA BURUNDI KUFUZU AFCON MWAKANI MISRI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23, kimeondoka leo asubuhi kwa ndege ya Air Tanzania kwenda Burundi ambako kesho itacheza na Burundi katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) Novemba mwakani nchini Misri.
  Msafara umeongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia na wachezaji wote wana morali kubwa kuelekea mchezo huo. 
  Wachezaji walioondoka ni makipa; Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili na Ally Salim, mabeki ni Ibrahim Hamad, Ally Msengi, Ayoub Masoud, Nickson Kibabage, Nickson Job, Ally Ally, Mohammed Abdallah na Adallah Shaibu ‘Ninja’.
  Viungo ni Oscar Masai, Abdallah Hamisi, Ismail Aidan na Salum Kihimbwa na washambuliaji ni Kelvin Nashon, Adam Salamba, Kelvin Sabato na Habib Kiyombo.
  .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 23 YAENDA KUCHEZA NA BURUNDI KUFUZU AFCON MWAKANI MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top