• HABARI MPYA

  Tuesday, November 13, 2018

  TFF YAWAFUNGIA MIAKA MITATU NA FAINI YA SH. MILIONI 2 KILA MMOJA VIONGOZI WAWILI WA MATAWI YANGA SC

  Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imewafungia wanachama wawili ambao ni Mwenyekiti wa Matawi wa Yanga, Bakili Makele na Katibu wake, Boaz Kupilika kutojihusisha na masuala ya michezo kutokana na utovu wa nidhamu.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF, Hamidu Mbwezeleni amesema kwamba wanachama hao wamefungiwa kifungo cha miaka mitatu kila mmoja kutojihusisha na masuala ya michezo huku wakitakiwa kulipa faini ya shilingi sh. milioni 2 kila mmoja kutokana na  kuhamasisha  wanachama kutofanya uchaguzi.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF, Hamidu Mbwezeleni (katikati), akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam

  Mbwezeleni amesema kwamba hatua hiyo imefikiwa baada ya wanachama hao Kupinga maelekezo ya Serikali na TFF kinyume na Katiba ya Yanga mwaka 2010 ibara ya 1 kifungu cha 6 kinachoitaka Yanga kuheshimu Katiba, kanuni, maagizo na maamuzi ya TFF na kuhakikisha kuwa zinaheshimika na wanachama kinyume ibara ya 50 (6), (1), (2) na katiba ya TFF ya mwaka 2013 kama ilivyorekebishwa 2015.
  Sababu nyingine ni kuitisha mkutano wa hadhara na kuongea maneno ambayo yana mgongano wa kimaslahi na TFF kinyume na ibara ya 50(6) ya Katiba ya TFF ya mwaka 2013, kama ilivyorekebishwa 2015 
  “Tumewafungia Bakili Makele na  Boaz Kupilika  kwa muda wa miaka mitatu kutojihusisha na masuala ya michezo ndani na nje ya nchi na kutoa faini ya shilingi milioni mbili kutokana na kusigana katiba ya Yanga pamoja na TFF.
  “Tumewafungia kwa makosa mawili ya kupinga maamuzi na maelekezo ya TFF ya uchaguzi wa klabu ya Yanga, pia kuongea maneno yenye mgongano na maslahi ya TFF jambo ambalo si sahihi, wanatakiwa wakaisome katiba yao wenyewe ya Yanga waone inaeleza nini," alisema  Zembweleni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAWAFUNGIA MIAKA MITATU NA FAINI YA SH. MILIONI 2 KILA MMOJA VIONGOZI WAWILI WA MATAWI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top