• HABARI MPYA

  Wednesday, November 14, 2018

  SOLARI ATHIBITISHWA KUWA KOCHA MPYA WA REAL MADRID HADI MWAKA 2021

  Muargentina Santiago Solari amethibitishwa rasmi kuwa kocha mpya Real Madrid hadi mwaka 2021 


  MATOKEO YA SOLARI TANGU APEE TIMU 

  Oktoba 31 - Melilla 0-4 Real Madrid
  Novemba 3 - Real Madrid 2-0 Real Valladolid
  Novemba 7 - Plzen 0-5 Real Madrid
  Novemba 11 - Celta Vigo 2-4 Real Madrid 
  KLABU ya Real Madrid imemthibitisha Santiago Solari kuwa kocha wake mpya kwa kumsainisha mkataba wa miaka wa miwili na nusu.
  Solari alipewa majukumu ya kufundisha kikosi cha kwanza cha Real Madrid wiki mbili zilizopita na kuwa na mwanzo mzuri kuliko kocha yeyote mpya katika historia ya miaka 116 ya klabu hiyo.
  Mechi zake nne za mwanzo zote ameshinda akifunga jumla ya mabao 15 na kufungwa mawili tu na kwa sababu hiyo wachezaji hawakuwa na shaka kupewa mkataba rasmi kwa mwalimu huyo Muargentina mwenye umri wa miaka 42.
  Jumanne Madrid ilisema katika taarifa yake: "Bodi ya Real Madrid katika kikao chake cha Novemba 13, 2018, imekubali kumtaja Santiago Solari kuwa kocha mkuu wa kikosi cha kwanza hadi Juni 2021,".
  Hiyo inamfanuya Solari awe kocha wa 13 katika zama za Rais, Florentino Perez ambaye alipewa madaraka kwa mara ya kwanza mwaka 2000, akaondoka 2006, na kurejea 2009.
  Atakuwa analipwa kiasi cha Pauni Milioni 5.2 kwa msimu kurithi majukumu ya mtangulizi wake, Julen Lopetegui hii ikiwa mara yake ya kwanza kufundisha timu ya wakubwa baada ya misimu mitatu ya kuwa na timu ya vijana ya klabu hiyo.
  Real Madrid bado wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa La Liga, lakini wanazidiwa pointi nne tu na vinara, Barcelona.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SOLARI ATHIBITISHWA KUWA KOCHA MPYA WA REAL MADRID HADI MWAKA 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top