• HABARI MPYA

  Thursday, November 15, 2018

  KOCHA SHIME ANAAMINI VIJANA WAKE U23 WATAWAGEUZIA KIBAO WARUNDI MECHI YA MARUDIANO KUFUZU AFCON U23

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23, Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ amesema anaweza kuwatoa Burundi katika mbio za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U23) mwakani nchini Misri.
  Tanzania jana ilichapwa mabao 2-0 na wenyeji, Burundi Uwanja wa Prince Rwegasore mjini Bujumbura katika mchezo wa kwanza wa mchujo kufuzu AFCON U23 iyakayifanyika Novemba mwakani nchini Misri.
  Mabao ya Burundi katika mchezo wa jana yalifungwa na Shaban Mabano kwa penalti dakika ya 59 na Cedric Mavugo‬ ‪dakika ya 79.
  Na baada ya mchezo huo, Shime alisema kwamba wamefungwa kutokana na makosa ambayo wanakwenda kuyafanyia kazi kabla ya mchezo wa marudiano na wanaamini watalipa kisasi nyumbani na kusonga mbele.
  Shime amesema kwamba Burundi wana timu nzuri na zaidi wachezaji wake walizidiwa kutokana na kucheza ugenini, lakini anaamini wakiwa nyumbani watafanya vizuri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA SHIME ANAAMINI VIJANA WAKE U23 WATAWAGEUZIA KIBAO WARUNDI MECHI YA MARUDIANO KUFUZU AFCON U23 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top