• HABARI MPYA

  Thursday, November 15, 2018

  KINDOKI AFIKISHA MABAO MANNE YA KUFUNGWA KATIKA MECHI SABA TU ALIZOCHEZA TANGU ASAJILIWE YANGA SC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIPA Klaus Kindoki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), jana amefikisha mabao manne ya kufungwa Yanga SC katika mechi ya saba tu tangu asajiliwe Julai mwaka huu.
  Kindoki, kipa mtanashati alifungwa bao la nne jana katika sare ya 1-1 na Reha FC ya Temeke katika mchezo wa kirafiki uliofanyika wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Klaus Kindoki jana amefikisha mabao manne ya kufungwa tangu asajiliwe Yanga SC Julai mwaka huu

  REKODI YA KLAUS KINDOKI YANGA 

  Yanga SC 1-0 Mawenzi Market (Hakufungwa Kirafiki Jamhuri Morogoro)

  Yanga SC 1-0 African Lyon (Hakufungwa Kirafiki Taifa)

  Yanga SC 4-3 Stand United (Alifungwa tatu na Felix Kitenge Ligi Kuu Taifa)

  Yanga SC 1-0 Coastal Union (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)

  Yanga SC 2-0 Mbao FC (Aliingiaa dakika ya 55 Beno alipoukia, hakufungwa, Ligi Kuu Taifa)

  Yanga SC 1-0 African Lyon (Hakufungwa Kirafiki Uhuru)

  Yanga SC 1-1 Reha FC (Alifungwa moja kirafiki Uhuru)

  Na aliyemfunga bao hilo ni Rashid Madebe aliyesajiliwa kutoka Lipuli FC ya Iringa, wakati bao la Yanga SC lilifungwa na kiungo chipukizi, Maka Edward.
  Na katika mechi saba alizodaka Yanga, Kindoki ameruhusu mabao katika mechi mbili tu, kabla ya jana alifungwa mabao mengine yote matatu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Stand United na mshambuliaji Mrundi, Alex Kitenge.
  Lakini mechi nyingine tano Kindoki ameweza kudaka bila kuruhusu mabao, ingawa bado udakaji wake umekuwa wa wasiwasi na zaidi alifutiwa makosa na walinzi wake.
  Kindoki alisajiliwa kwa matumaini makubwa Yanga kama mbadala wa kipa Mcameroon, Youthe Rostand aliyeonekana kufungwa mabao rahisi.
  Hata hivyo, Mkongo huyo ameshindwa kumshawishi kocha Mkongo mwenzake, Mwinyi Zahera kumpa dhamana ya kulinda lango la Yanga mbele ya mzalendo, Benno Kakolanya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KINDOKI AFIKISHA MABAO MANNE YA KUFUNGWA KATIKA MECHI SABA TU ALIZOCHEZA TANGU ASAJILIWE YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top