• HABARI MPYA

    Thursday, November 15, 2018

    BENKI YA TPB YATAMBUA MCHANGO WA WAANDISHI WA HAABRI ZA MICHEZO, YAWAPIGA JEKI TASWA FC KWA KUWAPA VIFAA VYA MICHEZO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    Dar es Salaam. Benki ya TPB imeendelea kuisadia  klabu ya  Waandishi wa habari za michezo  nchini (Taswa SC) baada ya kuikabidhi vifaa vya michezo ambavyo vitatumiwa na timu hiyo katika michezo yake mbalimbali.
    Akizungumza katika makabidhiano hayo jana mjini Dar es Salaam, Meneja  Mawasiliano wa  Benki ya TPB Chichi Banda alisema kuwa wamesaidia msaada huo ni sehemu ya shughuli za Benki na kutambua mchango mkubwa wa Waandishi wa Habari Nchini na muendelezo wao katika shughuli za kijamii ambapo mbali ya michezo, pia usaidia afya na elimu.
    Chichi alisema kuwa wamefariji kakutoa msaada huo kwaNTaswa SC ambayo mara kadhaa imekuwa ikitwaa ubingwa katika mashindano maalum ya vyombo vya habari yanayofanyika kila mwaka mkoani Arusha.



    Meneja Mawasiliano wa TPB Bank, Chichi Banda (Kulia) akikabidhi jezi kwa Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary jana 

    TPB Bank imetoa msaada ikiwa sehemu ya shughuli zao za kijamii. Alisema kuwa benki ya TPB ni wadau wakubwa wa michezo na mbali ya Taswa SC, pia usaidia timu nyingine.
    “Waandishi wa habari wameonyesha mfano mkubwa kwa kucheza soka na netiboli, wameamua kuhamasisha michezo katika jamii, kwa vitendo, hii imetupa faraja kubwa sana kwetu, ”alisema Chichi.
    Mwenyekiti waTaswa SC, Majuto Omary aliishukuru benki ya TPB kwa kuendelea kuwakumbuka na kuahidi kutumia vifaa hivyo  kwa umakini mkubwa na kushinda katika mechi zao mbalimbali.
    “Tunajivunia uwepo wa Benki ya  TPB kwa kuthibitisha kuwa ni benki halisi ya Watanzania, nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania kufungua akaunti zao katika benki hii na vile vilekuomba wadau wengine kufuata  mfano  kwa kuisaidiaTaswa SC ili iweze kufanikisha shughuli zake,” alisema Majuto.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BENKI YA TPB YATAMBUA MCHANGO WA WAANDISHI WA HAABRI ZA MICHEZO, YAWAPIGA JEKI TASWA FC KWA KUWAPA VIFAA VYA MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top