• HABARI MPYA

  Thursday, October 11, 2018

  YANGA SC WANAKWENDA ZANZIBAR KESHO KUCHEZA MECHI KUJIWEKA TAYARI NA MECHI ZIJAZO LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Yanga SC kinatarajiwa kuondoka asubuhi ya kesho kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Malindi FC ya huko.
  Yanga SC inataka kuutumia mchezo huo kuwaweka sawa wachezaji wake kipindi hiki Ligi Kuu ya Tanzania Bara imesimama kupisha mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Cameroon.
  Yanga SC imekuwa na rekodi nzuri katika Ligi Kuu msimu huu baada ya kushinda mechi zake zote tano za mwanzo kabla ya kulazimishwa sare ya 0-0 na mabingwa watetezi, Simba SC.

  Kwa sasa, Yanga SC wamejikusanyia pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, sawa na Singida United yenye wastani mdogo wa mabao na mechi tatu zaidi za kucheza - wakizidiwa pointi moja na Mtibwa Sugar waliocheza mechi tisa, wakati Azam FC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 18.
  Mabingwa watetezi, Simba SC wao wapo nafasi ya nne kwa pointi zao 14 baada ya kucheza mechi saba, wakizidiwa pointi moja na Azam FC iliyocheza mechi saba pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WANAKWENDA ZANZIBAR KESHO KUCHEZA MECHI KUJIWEKA TAYARI NA MECHI ZIJAZO LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top