• HABARI MPYA

  Friday, October 05, 2018

  YAHYA ZAYED ASEMA UHODARI WAKE KISOKA UMEONGEZEKA HADI KOCHA PLUIJM ANAFURAHIA KAZI YAKE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kuipa timu yake ushindi dhidi ya Tanzania Prisons, mshambuliaji wa Azam FC, Yahya Zayed, amesema anaamini kuwa kuna kitu kimeongezeka kwa upande wake kilichomshawishi kocha amuanzishe kwenye mchezo huo.
  Bao hilo linamfanya Zayed kufunga bao lake la kwanza msimu huu katika mechi yake ya kwanza kuanza kikosini msimu huu, akionekana kutengeneza kombinesheni nzuri na Donald Ngoma.
  Zayed amesema kwamba mchezaji anapocheza mechi ukianzia benchini na kocha akaamua kukuanzisha kikosi cha kwanza basi lazima kuna kitu kitakuwa kimemshawishi na kuamua kukuamini.
  “Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu bila yeye tusingeweza kufika hapa tulipofika leo na tusingeweza kupata ushindi leo (juzi) na nimefurahi sana kuipa timu yangu ushindi.
  “Kwa sababu kama ulivyoona kwenye mchezo wetu na Tanzania Prisons, timu ilijituma, tulijituma wote kiujumla tulicheza vizuri na tukaweza kufanikiwa kupata ushindi na najisikia vizuri sana,” alisema.

  Yahya Zayed (katikati) amesema kuna kitu kimeongezeka kwenye uchezaji wake 

  Zayed alizungumzia kuanza kwa mara ya kwanza kikosi cha kwanza na kudai kuwa; “Mimi nimejisikia vizuri kwa upande wangu kwa sababu nimeamini kama kuna kitu kimeongezeka kwa sababu unapotoka kila mechi unatokea benchi halafu unakuja kuaminiwa na kuanza kikosi cha kwanza inamaana kuna kitu umemuonesha mwalimu na umemshawishi kwa hiyo kaweza kukuamini na kuweza kukupanga kwenye kikosi cha kwanza kwa hiyo namshukuru Mwenyezi Mungu.”    
  Nyota huyo aliyemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, alitoa rai kwa wanafamilia wote wa Azam FC waendeleea kuwapa sapoti na waisoneshe utengano wowote huku akiwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi.
  “Mimi nawaomba mashabiki pamoja na viongozi na wafanyakazi wote wa Azam FC tusapotiane, tusitengane naamini tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu tuweze kuipatia timu yetu ushindi maana tupo kwenye lengo la kutafuta ubingwa…mashabiki wasichoke kuja kwa wingi,” alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YAHYA ZAYED ASEMA UHODARI WAKE KISOKA UMEONGEZEKA HADI KOCHA PLUIJM ANAFURAHIA KAZI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top