• HABARI MPYA

  Saturday, October 06, 2018

  SHAABAN IDDI CHILUNDA AINGIA AKITOKEA BENCHI CD TENERIFE YAFUMULIWA 4-1 SEGUNDA

  Na Mwandishi Wetu, MALLORCA
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Shaaban Iddi Chilunda usiku huu ameingia dakika ya 75 kwenda kuchukua nafasi ya Jose Naranjo, timu yake, CD Tenerife ikifungwa 4-1 katika mchezo wa ugenini wa Segunda dhidi ya wenyeji, Mallorca Uwanja wa Iberostar mjini Palma de Mallorca.  
  Chiliunda aliingia wakati tayari Tenerife imekwishapwa 3-1 na akashuhudia ikiongezwa la nne na kupoteza mchezo.
  Mabao ya Mallorca yamefungwa na Ariday Cabrera dakika ya nne, Junior Lago dakika ya 29, Abdon Prats dakika ya 56 na Alex Lopez dakika ya 81, wakati la Tenerife limefungwa na Salva Ruiz aliyejifunga dakika ya 52.

  Shaaban Iddi Chilunda ameingia dakika ya 75 kwenda timu yake, CD Tenerife ikifungwa 4-1 leo

  Hiyo inakuwa mechi ya pili kwa Chilunda kucheza Tenerife tangu asajiliwe Agosti kutoka Azam FC, baada ya Agosti 20 pia kutokea benchi dakika ya 85 kuchukua nafasi ya Filip Malbasic katika sare ya 1-1 ugenini na Gimnastic Tarragona Uwanja wa Tarragona.
  Chilunda mwenye umri wa miaka 20 yupo kwa mkopo wa miaka miwili Azam FC tangu Agosti mwaka huu akitoka kung’ara na kuibuka mfungaji bora wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu Kombe la Kagame.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHAABAN IDDI CHILUNDA AINGIA AKITOKEA BENCHI CD TENERIFE YAFUMULIWA 4-1 SEGUNDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top