• HABARI MPYA

  Friday, October 05, 2018

  SAMATTA AKUTANA NA ULINZI MKALI KRC GENK YACHAPWA 3-1 NORWAY, KUNDI LAO SASA KILA TIMU ‘SUMU’

  Na Mwandishi Wetu, SARPSBORG
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Samatta jana alicheza kwa dakika zote 90 timu yake, KRC Genk ikichapwa mabao 3-1 na wenyeji, Sarpsborg katika mchezo wa Kundi I Europa League Uwanja wa Sarpsborg mjini Sarpsborg nchini Norway.
  Samatta alikuwa chini ya ulinzi mkali jana wakati mabao ya Sarpsborg yakifungwa na Patrick Mortensen mawili dakika ya tano na 63 na Kristoffer Zachariassen dakika ya 54.
  Bao la kufutia machozi la KRC Genk usiku wa jana lilifungwa na Leandro Trossard dakika ya 49, akimalizia pasi ya Alejandro Pozuelo.

  Mbwana Samatta jana amecheza mechi ya 19 kwenye michuano ya Europa League akiwa amefunga mabao 12 tayari

  Sasa kila timu katika Kundi I imeshinda mechi moja na kufungwa mechi moja baada ya mechi mbili za mwanzo, huku Genk sasa ikikamata nafasi ya pili nyuma ya Sarpsborg na mbele ya Besiktas ya Uturuki na Malmo FF ya Sweden.
  Jana Samatta amecheza mechi ya 121 katika mashindano yote tangu amejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na amefunga jumla ya mabao 46.
  Katika Ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 94 na kufunga mabao 32, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 19 mabao 12.
  Kikosi cha Sarpsborg 08 FF kilikuwa; Vasyutin, Tamm, Halvorsen/Heintz dk72, Lund-Nielsen, Jorgensen, Thomassen, Zechariah, Tveita, Muhammed/Singh dk81, Mortensen na Askar.
  KRC Genk; Vukovic, Maehle, Dewaest, Lucumi, Nastic/Uron dk45, Berge, Malinovskyi/Heynen dk65, Pouelo, Trossard, Ndongala/Paintsil dk45 na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AKUTANA NA ULINZI MKALI KRC GENK YACHAPWA 3-1 NORWAY, KUNDI LAO SASA KILA TIMU ‘SUMU’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top