• HABARI MPYA

  Thursday, October 04, 2018

  RONALDO ATEMWA URENO BAADA YA TUHUMA ZA KUBAKA

  MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo ametemwa kwenye kikosi cha Ureno kitakachomenyana na Poland na Scotland baadaye mwezi huu.
  Nyota huyo wa Juventus, ambaye ameifungia timu yake ya taifa mabao 85 katika mechi 154, hajaitwa kwenye kikosi cha michuano ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya dhidi ya Poland na wa kirafiki dhidi ya Scotland.
  "Mbeleni hakuna kitakachomzuia Cristiano kutoa mchango wake timu ya taifa," amesema kocha Fernando Santos huku akiweka bayana kutomuita kwenye kikosi cha sasa.
  Cristiano Ronaldo ametemwa kikosi cha Ureno kitakachomenyana na Poland na Scotland 

  Cristiano Ronaldo akiwa na Kathryn Mayorga nchini Marekani anayedaiwa kumbaka mwaka 2009  

  Santos amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuwasiliana na Ronaldo na Mkuu wa Chama cha Soka Ureno. 
  Amekataa kusema sababu katika mazungumzo, akisema ni mambo binafsi na yasiyo ya kuwekwa hadharani.  
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amekanusha vikali madai kwamba alimbaka Kathryn Mayorga mmoja mjini Las Vegas, Marekani mwaka 2009.
  Kathryn Mayorga mwenye umri wa miaka 34 sasa, ni mwalimu ambaye alikuwa mwanamitindo mwenye mvuto wakati huo anaodai kubakwa.
  Amedai Ronaldo alimbaka bafuni katika hoteli ya Palms na Casino mjini Las Vegas mapema Juni 13, mwaka 2009 na nakala za Mahakama zimedai kwamba alimlazimisha japokuwa alikuwa akipiga kelele akisema 'Hapana, hapana, hapana!'
  Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 jana alikanusha vikali madai hayo akisema ni habari feki. 
  Miongoni mwa wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha Ureno kwa mechi hizi mbili ni Eder, aliyefunga bao la ushindi katika fainali ya Euro 2016 dhidi ya Ufaransa na Helder Costa wa Wolves, ambaye anaitwa kwa mara ya kwanza timu ya taifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO ATEMWA URENO BAADA YA TUHUMA ZA KUBAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top