• HABARI MPYA

  Monday, October 08, 2018

  ‘POPPA’ MBWANA SAMATTA AMEFANYA KAZI YAKE ULAYA, AMEFUNGA BAO LA KWANZA GENK IMESHINDA 5-1

  Na Mwandishi Wetu, GENT
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa Jumapili amefungua biashara nzuri ya mabao, timu yake KRC Genk ikishinda 5-1 ugenini dhidi ya AA Gent katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji dhidi ya GHELAMCO-Arena mjini Gent.
  Samatta, Nahodha wa Taifa Stars amefunga bao la kwanza dakika ya 17 kabla ya kubadilishwa dakika ya 74, nafasi yake akichukua mshambuliaji kinda wa miaka 22, Mdenmark Marcus Ingvartsen.
  Mabao mengine ya Genk yamefungwa na washambuliaji Mghana, kinda wa miaka 20 Joseph Paintsil dakika ya 18 na 73, Mkongo Dieumerci N'Dongala dakika ya 27 na kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy dakika ya 67, wakati la Gent limefungwa na beki Mfaransa Dylan Bronn dakika ya 39.

  Samatta amefikisha mechi 122 katika mashindano yote tangu amejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na amefunga jumla ya mabao 47.
  Katika Ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 95 na kufunga mabao 33, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 19 mabao 12.
  Kikosi cha AA Gent kilikuwa; Kalinic/Thoelen dk45, Rosted, Plastun, Verstraete, Chakvetadze, Odjidja, Limbombe/Esiti dk45, Awoniyi/Yaremchuk dk65, Dejaegere, Asare na Bronn.
  KRC Genk; Vukovic, Maehle, Aidoo, Lucumi, Uronen, Berge/Wouters dk83, Malinovskyi, Pozuelo, Ndongala/Fiolic dk76, Paintsil na Samatta/Ingvartsen dk72.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ‘POPPA’ MBWANA SAMATTA AMEFANYA KAZI YAKE ULAYA, AMEFUNGA BAO LA KWANZA GENK IMESHINDA 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top