• HABARI MPYA

  Wednesday, October 03, 2018

  POGBA APIGWA MARUFUKU KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

  Paul Pogba amepigwa marufuku na Manchester United kuzungumza na vyombo vya Habari 


  MSIMU WA POGBA

  Ligi Kuu mechi: 7
  Mabao ya Ligi Kuu: 2, 
  Pasi za mabao Ligi Kuu: 1
  Pasi zilizofika: Asilimia 82.7 
  Mechi za Ligi ya Mabingwa: 2
  Mabao Ligi ya Mabingwa: 2
  Pasi za mabao Ligi ya Mabingwa: 1 
  Pasi zilizofika: Asilimia 85.5  
  KIUNGO Paul Pogba amepigwa marufuku na klabu yake, Manchester United kuzungumza na vyombo vya Habari kufuatia kauli tata alizowahi kutoa.
  Pogba aliibua mijadala juu ya mustakabali wake Old Trafford baada ya kuiongoza timu kama Nahodha katika ushindi dhidi ya Leicester City mwanzoni mwa msimu mwezi Agosti kwa kusema hahofii kuzungumzia kutaka kwake kujiunga na Barcelona.
  Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa dau la rekodi ya dunia wakati huo, Pauni Milioni 89 baada ya mechi na Wolves iliyomalizika kwa sare ya 1-1 mwezi uliopita alikosoa mbinu za kocha Jose Mourinho kwa kusema timu inatakiwa kushambulia ikiwa inacheza Uwanja wa Old Trafford.
  Na baada ya sare ya jana ya 0-0 dhidi ya Valencia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Pogba alikataa kuzungumza na Waandishi wa Habari waliokuwa wanamsubiri akiwaambia: "Nimeambiwa siruhusiwi,".
  Hii ni mara ya kwanza United imeamua kumnyamazisha Pogba ambaye amekuwa akizungumza mno na vituo vya Televisheni mbalimbali tangu ashinde Kombe la Dunia na Ufaransa.
  Mwezi uliopita alikiambia kituo cha Televisheni cha Ujerumani: "Mustakabali wangu kwa sasa upo Manchester. Bado nina mkataba, nacheza huko kwa sasa, lakini nani anajua kitakachotokea baadaye?,".
  Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 anataka kuondoka United kuhamia Barcelona miaka miwili na nusu tu tangu arejee Old Trafford kutoka Juventus kwa dau la rekodi ya dunia wakati huo.
  Pogba amekwishaamua kuondoka Manchester United hata kama Mourinho atafukuzwa kufuatia kukwaruzana na kocha huyo mara kadhaa. 
  Wiki iliyopita Mourinho alimvua cheto cha Unahodha Msaidizi wa klabu Pogba kwa sababu alishindwa kuonyesha tabia za kiuongozi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POGBA APIGWA MARUFUKU KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top