• HABARI MPYA

  Sunday, October 07, 2018

  MWADUI FC YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU, YAIPIGA BIASHARA MARA 2-0 PALE PALE MUSOMA

  Na Mwandishi Wetu, MUSOMA
  TIMU ya Mwadui FC imepata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Biashara United mabao 2-0 Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara. 
  Pongezi kwa wafungaji wa mabao hayo katika mchezo wa leo, Abdulrahman Mussa dakika ya 70 na Juhudi Philemon dakika ya 90 na ushei.
  Sasa Mwadui FC kutoka wilayani Kishapu mkoani Shinyanga inafikisha pointi tano baada ya kucheza mechi nane na Biashara United inabaki na pointi zake sita katika mechi ya nane.

  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, JKT Tanzania imelazimishwa sare ya 1-1 na Alliance FC ya Mwanza Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu na wa mwisho leo unafuatia Saa 1:00 usiku wa leo kati ya wenyeji, Yanga SC na Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWADUI FC YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU, YAIPIGA BIASHARA MARA 2-0 PALE PALE MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top