• HABARI MPYA

  Wednesday, October 10, 2018

  MTIBWA SUGAR WAANZA MAANDALIZI YA KWENDA KUKUSANYA POINTI KANDA YA ZIWA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Mtibwa Sugar kimeanza mazoezi yake leo baada ya kumaliza mapumziko waliyopewa na benchi la ufundi, mapumziko hayo yalianza baada ya mchezo dhidi ya KMC siku ya Jumamosi na leo kikosi cha wana tam tam kilifanya mazoezi jioni.
  Kikosi cha wana tam tam kesho kinataraji kuendelea na mazoezi ya kujiweka sawa na kesho asubuhi kikosi cha wana tam tam wataingia Gym kwa ajili ya kujiweka fiti.
  Kikosi cha wana tam tam kitaendelea na mazoezi yake katika dimba la Manugu kikijiwinda na maandalizi ya ligi kuu bara (TPL) kwa ajili ya mzunguko wa 10, Mtibwa Sugar itasafiri hadi kanda ya ziwa kwa ajili ya michezo 2 ya ligi kuu bara (TPL) dhidi ya Mbao tarehe 21.10.2018 na Stand United tarehe 24.10.2018.

  Kuna baadhi ya wachezaji waliokosa mazoezi ya leo ni Riphat Khamis aliyeumia katika mchezo dhidi ya Mbeya City , Ally Shomary na Ismail Aidan Mhesa ambaye anataraji kesho kuanza mazoezi kwa mujibu wa ripoti ya daktari.
  “Riphati kakosekana anaumwa enka bado maumivu yake yalikuwa makubwa , Ally Shomary naye bado yupo chini ya uangalizi wa daktari hivyo haja anza mazoezi na Ismail Mhesa naye kakosekana leo tu ila kesho daktari ametupa report nzuri atakuwa nasi mazoezini ” David Bugoya (Manager)
  Mtibwa Sugar hadi sasa inashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu bara (TPL) baada ya kucheza michezo 9 na kufanikiwa kukusanya pointi 17 huku ikiwa pointi 1 nyuma ya Azam Fc yenye pointi 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAANZA MAANDALIZI YA KWENDA KUKUSANYA POINTI KANDA YA ZIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top